UEFA: Manchester City yaibamiza Monaco 5-3

Leroy Sane akipachika goli la nne dhidi ya Monaco
Maelezo ya picha,

Leroy Sane akipachika goli la nne dhidi ya Monaco

Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya mechi iliyochezwa usiku wa kuamkia leo Jumatano ni Manchester City imeibuka mshindi kwa mabao 5 kwa 3 dhidi ya Monaco.

Mechi nyingine Bayer Leverkusen ilitandikwa 4-2 na Atletico de Madrid.

Michuano hiyo ya Ulaya itaendelea tena leo kwa michezo mingine miwili ya Europa Ligi kupigwa.

FC Seville watakua nyumbani kuwaalika mabingwa wa ligi kuu England wenye mwendo wa kusuasua Leicester City.

Wareno wa FC Porto watawakaribisha vibibi vizee vya Torino, Juventus.