Guardiola: Man City sharti tufunge mabao mengi Monaco

Pep Guardiola Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sergio Aguero sasa amefunga mabao mawili na zaidi katika mechi saba msimu huu

Manchester City "wataondolewa" kwenye michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya iwapo hawatafunga katika mechi ya marudiano hatua ya 16 bora dhidi ya Monaco, meneja wao Pep Guardiola amesema.

City walitoka nyuma mara mbili na hatimaye wakafanikiwa kuwalaza viongozi hao wa ligi ya Ufaransa 5-3 mechi ya kusisimua iliyochezewa uwanja wa Etihad.

Mechi ya marudiano itachezwa 15 Machi.

"Tutasafiri Monaco na kufunga mabao mengi kadiri iwezekanavyo," Guardiola alisema baadaye.

"Hilo ndilo lengo langu. Ni vigumu kwetu kusonga tusipofunga bao."

Monaco waliongoza 2-1 na 3-2 kabla ya City kujikwamua na kupata ushindi.

Mechi hiyo inaongoza kwa kufungwa mabao mengi miongoni mwa mechi za mkondo wa kwanza hatua ya muondoano katika miaka 25 ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Guardiola anatarajia mechi iwe wazi sana klabu hizo zitaapokutana tena.

Anahisi hiyo ndiyo njia bora zaidi ya kukabiliana na mashambulio makali ya Monaco ambao wamefunga mabao 76 mechi 26 za ligi Ufaransa msimu huu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester City wamekomboa penalti zote tano zilizopigwa karibuni zaidi dhidi yao Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (mbili na Caballero, tatu na Joe Hart)

"Wanacheza kwa njia hiyo - watashambulia na kushambulia," alisema Guardiola.

"Tutahitaji kujilinda zaidi lakini tutapata nafasi. Nina uhakika kuhusu hilo.

"Je, nina furaha timu yangu ikifungua mchezo? Ndio. Sana."

Rekodi ya Pep Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
Msimu Klabu Hatua Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
2008-09 Barcelona Fainali (wakawalaza Man Utd 2-0)
2009-10 Barcelona Nusufainali (3-2, wakashindwa na Inter)
2010-11 Barcelona Fainali (wakalaza Man Utd 3-1)
2011-12 Barcelona Nusu fainali (3-2, wakalazwa na Chelsea)
2013-14 Bayern Munich Nusu fainali (5-0 , wakalazwa na Atletico Madrid)
2014-15 Bayern Munich Nusu fainali (5-3 , wakalazwa na Barcelona)
2015-16 Bayern Munich Nusu fainali (2-2 sare na Atletico. Atletico wakasonga kwa magoli ya ugenini)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii