Kipa apigwa marufuku kwa kuachia mabao 3 kwa makusudi Vietnam

Mlinda lango afungwa bao la penalti
Maelezo ya picha,

Mlinda lango afungwa bao la penalti

Mlinda lango wa timu ya Vietnam amepigwa marufuku kucheza soka kwa miaka miwili kwa kuongoza ule unaoitwa mgomo mgando wakati wa mechi.

Pamoja na wachezaji wa timu yake walisimama bila kutingisika hata kidogo wakitazama timu pinzani Ho Chi Minh City kuifunga mabao matatu ya dakika za lala salama kabla ya mechi kukamilika

Walikuwa wakipinga uamuzi wa refa kuipatia timu hiyo penalti iliyokumbwa na utata.

Picha za video zilimuonesha akilipa mgongo bao la kwanza la penalti.

Mojawapo ya mabao mengine mawili yaliyofuata aliyakwepa hasa kwa kwa kuruka kando kwa makusudi.

Shirikisho la kandanda la Vietnam limempiga marufuku miaka miwili pia nahodha wa timu hiyo likisema mgomo huo ulionesha utovu wa nidhamu kwa refa.