Wayne Rooney kuihama Manchester United?

Wayne Rooney anadaiwa kutaka kuihama Manchester United
Maelezo ya picha,

Wayne Rooney anadaiwa kutaka kuihama Manchester United

Kumekuwa na taarifa kuhusu uwezekano wa Wayne Rooney kuihama Manchester United na kuelekea nchini China mwezi huu.

Lakini Kocha wa klabu ya Tianjin Quanjian ya nchini China, Fabio Canavaro amesema mazungumzo hayakuendelea.

Imefahamika kuwa kuna uwezekano wa kufanikisha mpango huo juma lijalo ni finyu na matarajio ni kuwa Rooney ataendelea kubaki Manchester united kwa kipindi chote cha msimu

Hata hivyo, upo uwezekano wa kuondoka kwa Rooney akiiacha Old Trafford baada ya kuichezea manchester united kwa miaka 13.

Matamanio ya Wyne Rooney inaeleweka ni kubaki na Manchester United mpaka mkataba wake utakapokwisha mwaka 2019, kutopata nafasi katika kikosi cha kwanza kimekuwa kikisabisha rooney kutaka kuiacha Manchester United