Manchester United washinda na kusonga Europa League

Henrikh Mkhitaryan alifunga lakini akaondoka uwanjani dakika tisa baadaye

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Henrikh Mkhitaryan alifunga lakini akaondoka uwanjani dakika tisa baadaye

Manchester United walifika hatua ya 16 bora katika ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Saint-Etienne Jumatano.

Hata hivyo, mfungaji bao wao Henrikh Mkhitaryan huenda akakosa mechi ya Kombe la EFL Jumapili baada ya kuumia na kulazimika kuondoka uwanjani wakati wa mechi hiyo.

United walikuwa mbele 3-0 kutokana na ushindi wa mechi ya mkondo wa kwanza, mabao yote yakitoka kwa Zlatan Ibrahimovic.

Kwenye mechi ya Jumatano iliyochezewa Ufaransa, Mkhitaryan alifunga dakika ya 16 kutoka kwa krosi ya Juan Mata.

Muda mfupi baadaye hata hivyo, mchezaji huyo kutoka Armenia alionekana kuumia misuli ya paja na kulazimika kuondoka wuwanjani.

Beki wao Eric Bailly pia alifukuzwa uwanjani dakika ya 63 baada ya kuonesha kadi ya pili ya njano.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mkhitaryan amefungia Manchester United mabao sita

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Paul Pogba alitawazwa mchezaji bora wa mechi hiyo