Santi Cazorla: Nyota wa Arsenal nje hadi mwisho wa msimu

Chanzo cha picha, Rex Features
Cazorla alijiunga na Arsenal akitokea Malaga kwa £15m mwaka 2012
Kiungo wa kati wa Arsenal Santi Cazorla atakaa nje ya uwanja kwa kipindi chote kilichosalia cha msimu huu kutokana na jeraha la kifungo cha mguu.
Cazorla hajacheza hadi alipochechemea na kuondoka uwanjani mechi ya hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Ludogorets uwanajni Emirates mwezi Oktoba.
Alifanyiwa upasuaji Desemba na meneja wa Gunners Arsene Wenger alitumai mchezaji huyo wa miaka 32 angerejea kabla ya msimu kumalizika.
Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania sasa ataangazia kujiweka sawa kurejea kwa ajili ya msimu ujao.