Fatuma Zarika: Ubingwa ninao lakini sikulipwa

Fatuma Zarika: Ubingwa ninao lakini sikulipwa

Fatuma Zarika wa Kenya mwaka jana aliweka historia kuwa bondia wa kwanza mwanamke wa Afrika Mashariki kushinda taji la dunia katika ndondi za kulipwa.

Zarika alimshinda kwa pointi Alicia Ashley wa Jamaica nchini Marekani, na kutwaa ubingwa wa dunia uzani wa super-bantam chama cha WBC.

Lakini mpaka sasa Fatuma hajalipwa tangu anyakue taji hilo.

Katika mazungumzo yake na John Nene, Zarika anatueleza mengi jinsi mabondia wa kutoka nje wanavyonyanyashwa nchini Marekani.