Leicester City yamtimua Kocha wake

Ranieri alikuwa Kocha wa Leicester tangu Julai 2015

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha,

Ranieri alikuwa Kocha wa Leicester tangu Julai 2015

Bingwa mtetezi wa ligi kuu England Leicester City imemtimua Kocha wake muitaliano Claudio Ranieri, ikiwa ni miezi tisa baada ya kuiwezesha kupata ubingwa wa Ligi kuu.

Leicester iko katika nafasi ya 17, na ikipoteza alama moja tu itakuwa kwenye mstari wa kushuka daraja.

Kutimuliwa kwa kocha huyo kumekuja saa 24 baada ya kichapo cha magoli 2-1 walichopata kutoka kwa FC Seville.

Leicester City msimu uliopita ilitwaa ubingwa kwa zaidi ya alama 10 mbele, lakini msimu huu, mpaka sasa wamecheza michezo 25 ya ligi na kushinda mitano pekee, na imesalia michezo 13 ligi kuisha.