Kenya kucheza dhidi ya Hull City Uingereza

Uwanja wa Hull City nchini Uingereza
Maelezo ya picha,

Uwanja wa Hull City nchini Uingereza

Timu inayoshirikisha wachezaji wa Kenya kutoka ligi ya soka ya taifa hilo Watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Klabu ya Uingereza Hull City.

Mechi hiyo inayofadhiliwa na SportPesa- kampuni ya kamare kutoka Kenya ilioshinda haki ya kuifadhili timu hiyo ya Uingereza kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Timu ya Kenya yenye wachezaji 18 imepiga kambi katika maeneo ya Kaskazini mwa Uingereza tangu wiki iliopita ikijifunza mbinu tofauti za soka ya kulipwa.

Siku ya Jumapili Hull City walicheza dhidi ya Burnley ambapo walitoka sare ya 1-1.

Kocha wa timu ya taifa ya Kenya Stanley Okumbi anasema kuwa wachezaji wa Kenya wamenufaika sana na ziara hiyo.

Maelezo ya picha,

Kocha wa Kenya Stanley Okumbi kuiongoza Kenya dhidi ya Hull City

''Wachezaji wamenufaiki sana na mazoezi na wamepata ujuzi chungu nzima ambao watautumia katika siku za usoni na katika mechi dhidi ya Hull City''.