Timu ya akiba ya Hull City yailaza Kenya

Wachezaji wa timu ya Hull City nchini Uingereza

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wachezaji wa timu ya Hull City nchini Uingereza

Bao la dakika za mwisho la Humphrey Mieno halikutosha kuwaokoa wachezaji wa timu ya Sport pesa kutoka Kenya ambao walilazwa na timu ya Hull City nchini Uingereza katika mechi ya kirafiki .

Bao la kujifunga la beki Harun Shakava katika kipindi cha pili liliigharimu Kenya ambayo ilikuwa imeahidiwa kitita cha shilingi milioni 1.1 iwapo wangeishinda timu hiyo ya Ligi ya Uingereza.

Hull City walikuwa juu kwa bao moja lililofungwa na Elliot Holmes katika dakika ya 11.

Kocha Stanley Okumbi alianzisha nyota wake wote huku mshambuliaji Allan Wanga akiongoza safu yake ya mashambulizi.

Waandalizi hatahivyo waliwasilisha wachezaji watano pekee kutoka kikosi cha kwanza Josh Tymon,Greg Olley,Max Sheaf,Greg Luer na Jarrod Bowen.

Daan Windas ambaye mchezo wake 2008 uliisaidia timu hiyo kupanda daraja alichezeshwa kama mchezaji wa ziada.