Mchezaji wa Togo amsaidia mwenzake kupumua

Kone akimsaidia kipa Berkovic

Chanzo cha picha, Bohemians

Maelezo ya picha,

Kone akimsaidia kipa Berkovic

Mshambuliaji wa timu ya Togo Francis Kone aliokoa maisha ya kipa Martin Berkovec ambaye nusra ameze ulimi wake wakati wa mechi ya ligi ya Czech.

Kone alichukua hatua za haraka baada ya Berkovec kugongana na mwenzake Daniel Krch.

Alitumia vidole vyake kuutoa ulimi wa kipa huyo aliyekuwa anapigania hewa na kumwezesha kupumua.

Berkovec baadaye alichapisha katika mtandao wake wa Facebook akisema :Ningependa kumshukuru Francis Kone kwa kuniokoa kwa dharura.

Kone baadaye alitajwa kuwa shujaa baada ya kisa hicho