Mshambuliaji wa DR Congo kutocheza kwa wiki sita

Mshambuliaji wa klaby ya Hull City Dieumerci Mbokani kulia Haki miliki ya picha PA
Image caption Mshambuliaji wa klaby ya Hull City Dieumerci Mbokani kulia

Mshambuliaji wa klabu ya Hull City Dieumerci Mbokani hatocheza kwa kipindi cha wiki sita baada ya kupata jeraha la paja.

Mshambuliaji huyo wa DR Congo mwenye umri wa miaka 31 ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Dynamo Kiev alibadilishwa wakati wa sare ya 1-1 dhidi ya Burnley.

Hull pia imethibitisha kuwa jeraha la goti alilopata beki Harry Maguire wakati wa mechi dhidi ya Burnley sio baya sana zaidi ya ilivyodhaniwa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 huenda akapona tayari kwa safari ya kueleka Leicester City siku ya Jumamosi.