Uingereza na Urusi kurekebisha uhusiano

Urusi
Image caption Urusi

kamati ya bunge la Uingereza imetoa mwito kwa serikali kutumia mwaka ujao kutumia michuano ya kombe la dunia itakayo fanyika nchini Urusi kurekebisha uhusiano mbaya baina ya Uingereza na Moscow, kitendo kinachotafsiriwa kuwa haba tangu vita baridi.

Kamati ya mambo ya Nje ilionyesha wasiwasi wake endapo Urusi inastahili kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kutokana na rekodi mbaya iliyonayo kuhusiana na haki za binaadamu.

Ingawa kamati hiyo iliongeza kusema kwamba badala ya Uingereza kugomea mashindano, serikali inapaswa kutumia mwanya wa mashindano hayo kuboresha uhusiano wa mataifa hayo mawili, kwa kuongeza wafanyakazi wa kidiplomasia pamoja na ushirikiano wa polisi kujiandaa kwa lolote litakalojiri kutoka kwenye umati wa watu.