John Barnes awasili Tanzania

Tanzania Haki miliki ya picha Google
Image caption Mchezaji nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes (wa pili kushoto) akiwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere- VIP Terminal I na kupokelewa na wenyeji wake ambao ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said (wa pili kulia), Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba (kulia) pamoja na Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas (kushoto).

Mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa England na klabu ya Livepool, John Barnes amewasili nchini Tanzania.

Alipokelewa na wenyeji wake ambao ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said ,Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba pamoja na Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 100 ya benki ya Standard Chartered ambayo ni wadhamini wakuu wa klabu ya Liverpool. .

Bingwa wa Mashindano hayo atapata nafasi ya kwenda nchini Liverpool Uingereza.Timu zilizoingia fainali za mashindano hayo ya kikanda ni Azania Group ya Tanzania, Capital FM ya Kenya na Cocacola ya Uganda.

Barnes ambaye hii ni zaidi ya mara ya tatu anakuja Tanzania kwa shughuli mbalimbali za kijamii, hapa anazungumza na Waandishi wa Habari