Liverpool kukabana koo na Arsenal Anfield

Bellamy wa Arsenal akikabiliana na Coutinho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bellamy wa Arsenal akikabiliana na Coutinho

Nahodha wa klabu ya Liverpool Jordan Henderson atasalia nje na jeraha la mguu huku Daniel Sturridge akiuguza jeraha la kiuno.

Dejan Lovren hajacheza tangu tarehe 31 Januari lakini amerudi katika mazoezi na atakaguliwa kabla ya mchezo huo.

Mesut Ozil alikatiza mazoezi siku ya Alhamisi baada ya kuugua lakini anatarajiwa kucheza.

Aaron Ramsey na Laurent Koscielny wanarudi lakini Mohammed Elneny atauguza jeraha kwa wiki tatu.