Wezi wavunja nyumba ya John Terry na kuiba

John Terry na Mkewe
Image caption John Terry na Mkewe

Wezi wanaaminika kuvunja na kuingia katika nyumba ya aliyekuwa nahodha wa timu ya uingerewza John Terry wakati akiwa katika likizo ya kifamilia.

Maafisa wa polisi wa Surrey walithibitiha kwamba nyumba iliopo Oxshott ilivunjwa wikendi iliopita.

John Terry ameripotiwa kuishi katika nyumba ya vyumba saba nchini humo.

Msemaji wa kituo hicho cha polisi wa Surrey amesema kuwa : Tunaweza kuthibitisha kuwa wizi ulifanyika katika nyumba moja iliopo Moles Hill ,Oxshott usiku wa terehe 25 na 26 mwezi Februari .

Wezi hao wanadaiwa kuvunja na kuuingia katika nyumba hiyo na kuiba vitu vyenye thamani wakati ambapo mchezaji huyo wa Chelsea mwenye umri wa miaka 36 alikuwa ameenda likizo na watu wa familia akiwemo mkewe Toni kulingana na ripoti za gazeti la The Sun.