Manchester United wasalia nambari 6 baada ya sare ya 1-1

Mchezaji wa manchester United akifanya shambulizi katika lango la Bournemouth, mechi hiyo iliisha 1-1 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji wa manchester United akifanya shambulizi katika lango la Bournemouth, mechi hiyo iliisha 1-1

Klabu ya Manchester United imesalia katika nafasi ya sita katika ligi ya Uingereza baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya wageni wao wa Bournemouth waliosalia na wachezaji 10 uwanjani.

Mechi hiyo ilikumbwa na visa vya ukosefu wa nidhamu uliomuhusisha mshambuliaji wa United Zlatan Ibrahimovic na Tyrone Mings wa Bournemouth.

Visa vyote viwili vilitokea mwisho wa kipindi cha kwanza cha mechi baada ya wachezaji hao kuonywa na refa Kevin Friend.

Alipewa kadi ya njano ambapo Friend aligundua ni yake ya pili na hivyobasi kutakiwa kutoka uwanjani.

Marcos Rojo aliiweka kifua mbele Manchester United kabla ya Bournemouth kusawazisha.

Baadaye mshambuliaji wa United Ibrahimovic alishindwa kufunga mkwaju wa penalti baada ya beki wa Bournemouth kuunawa mpira langoni.