Tottenham yaichapa Everton-Epl

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Harry kane,mchezaji wa Tottenham

Klabu ya soka ya Tottenham wakiwa nyumbani kwao dhidi ya Everton walifanikiwa k kuchomoza na ushindi wa mabao 3-2.

Magoli ya Tottenham katika mchezo huo yalifungwa na wachezaji Harry kane akifunga magoli mawili, bao la tatu na la mwisho likifungwa na Delle Alli .

Kwa upande wa Everton magoli yao yamefungwa na wachezaji Romeo Lukaku na Enner Valencia.

Katika mchezo wa pili Sunderland wakiwa wenyeji wa Manchester city mchezo ulimalizika kwa Manchester city kutoka na ushindi wa mabao 2-0.

Kwa matokeo hayo Chelsea kabla ya ya mchezo wao wa leo bado ni vinara wa ligi wakiwa na alama 63,Tottenham 56,Manchester city 55,Liverpool 52 na Arsena 50.

Leo jumatatu West Ham United wanacheza dhidi ya vinara wa ligi Chelsea.