Yanga yabanwa mbavu na Mtibwa Sukari

Haki miliki ya picha Google
Image caption Simon Msuva,mchezaji wa Yanga

Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania bara Yanga, jana wameshindwa kuing'oa vinara ligi hiyo Simba baada ya kutoka Sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar Jamhuri Mjini Morogoro.

Yanga wangeweza kushinda Mechi hii baada ya kupewa Penati ya Dakika ya 34 lakini Mchezaji wao Simon Msuva akashindwa kuifunga Penati hiyo.

Kwa Matoke ohayo Yanga wanabaki Nafasi ya Pili nyuma ya Simba ambao wako alama 2 mbele yao baada ya Jumamosi kutoka Sare 2-2 na Mbeya City.

Katika Mechi nyingine iliyochezwa jana African Lyon iliitungua Mwadui FC 1-0 .

Ligi hiyo ya Tanzania bara inatarajia kuendelea tena leo Jumatatu Machi kwa mchezo mmoja ambapo Ndanda wanakuchele wanawakaribisha maafande wa Ruvu Shooting.