Kenya yanyakua taji la trophy katika raga Marekani

Wachezaji wa Kenya wa timu ya wachezaji saba kila upande wakisherehekea ushindi wao
Image caption Wachezaji wa Kenya wa timu ya wachezaji saba kila upande wakisherehekea ushindi wao

Timu ya Kenya ya raga ya wachezaji saba kila upande imejinyakulia taji la trophy mjini Las Vegas baada ya kuishinda Samoa 21-14 katika fainali iliochezwa uwanja wa Sam Boyd.

Ni kombe la pili la timu ya shujaa baada ya kushinda kombe kama hilo katika mashindano ya Wellington sevens mnamo mwezi Januari 29.

Nahodha Andrew Amonde aliongoza kikosi hicho baada ya kufunga trai mbili huku Collins Injera akiongeza trai nyengine kwa kupiga mkwaju wa sammy Okoth.

Ikielekea fainali Kenya iliicharaza Ufaransa 14-7 huku samoa ikiishinda Scotland 24-0 katika semi.

Amonde alikuwa na haya ya kusema: Hatukecheza vyema sana lakini ni vizuri kupata kitu.

Nashkuru mashabiki ,tunajua tuna zaidi na tutategemea ushindi huo huko mjini Vancouver.

Nyota mwenye kasi zaidi Injera alipata mpira na kuipta safu ya ulinzi ya Samoa kwa trai yake ya 242 huku Olich akifunga na kuiweka Kenya kifua mbele 7-0.