Wenger: Hatuna mgogoro wowote na Alexi Sanchez

Arsene Wenger
Image caption Arsene Wenger

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ripoti kwamba kulikuwa na mgogoro katika mazoezi kati ya Alexi Sanchez na wachezaji wenzake ni uongo.

Sanchez anaaminika kugombana na wachezaji wenzake baada ya kuondoka katika mazoezi katikati kabla ya mechi ya Jumamosi walioshindwa na Liverpool.

Alikabiliwa na wachezaji wenzake baada ya kurudi katika chumba cha kubadilisha jezi huku kukiwa na hasira.

Lakini Wenger alisema sijui kama kuna kitu kilitokea.

Sanchez aliwachwa nje ya kikosi cha kwanza cha Arsenal uwanjani Anfield lakini aliingia na kuitengenezea bao timu yake katika mechi ambapo Arsenal ilipoteza kwa 3-1.

Image caption Alexi Sanchez

''Ni mchezaji mwenye kujitwika majukumu na mara nyengine huwa na tabia nzito lakini nimejionea kama hayo katika vikosi vingi''.

Wenger alikuwa akizungumza kabla ya mechi ya marudiano ya kombe la vilabu bingwa Ulaya siku ya Jumanne wakiialika Bayern ambayo inaongoza 5-1.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 , kocha huyo alisema: kwa kweli kama mchezaji mwengine yeyote yule.