FA - kuwaadhibu Ibrahimovic , Mings

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji Ibrahimovic na Ming wakiwa pamoja na mwamuzi Kevin Friend

Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic na Beki wa Bournemouth Tyrone Mings wamefunguliwa Mashitaka na chama soka cha England (FA) kwa Mchezo usio wa kiungwana .

Wachezaji hao walichezeana faulo mara kwa mara kwenye Mechi ya Jumamosi ligi kuu ya England ambapo timu hizo zilitoka Sare 1-1 katika Uwanja wa Old Trafford ambapo Mings alimchezea faulo kwa kumkanyaga kichwani Ibrahimovic aliyekuwa ameanguka chini katika Dakika ya 44 na Dakika 2 baadaye Ibrahimovic akijibu kwa kumpiga kiwiko Mings wakati akipiga Kichwa Mpira wa Kona.

Wachezaji hao wamepewa muda hadi kufikia leo kujibu Mashitaka yao, FA imeeleza Matukio hayo waliyoshitakiwa nayo hayakuonwa na mwamuzi Kevin Friend lakini yalinaswa kwenye Video wakati mchezo ukiendelea.

Kwa mujibu wa Kanuni za FA, Mchezaji kumpiga Kiwiko na Kumkanyaga mchezaji mwezake makusudi ni faulo ambazo zinastahili kutolewa kadi nyekundu na pia Kifungo cha kusimamishwa kucheza Mechi 3.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mings akiwa ameanguka

Ikiwa Wachezaji hao watapatikana na hatia basi Ibrahimovic ataikosa Mechi ya Robo Fainali ya FA CUP dhidi ya Chelsea na Mechi ya Ligi dhidi ya Middlesbrough na West Bromwich Albion.

Kwa upande wake Mings ,yeye atazikosa Mechi za Bournemouth dhidi ya West Ham, Swansea City na Southampton na pengine mechi nyingine zaidi ya hizo.