Arsenal kusonga mbele leo ?

Haki miliki ya picha Google
Image caption Logo ya UEFA

Mechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya timu 16 ya UEFA CHAMPIONI LIGI, zinaanza kuchezwa leo Jumanne Machi 7 kwa Mechi 2.

Huko Emirates Jijini London, Wenyeji Arsenal wanapaswa kupindua kipigo cha 5-1 walichoshushiwa na Bayern Munich katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Ujerumani.

Ili kufuzu kuingia Robo Fainali, Arsenal wanapaswa kufanya kitu ambacho hakijawahi kufanyika kwa kushinda 4-0 au kwa idadi nyingine ya Mabao ilimradi tofauti ya Magoli iwe 4-0.

Mechi ya Pili ya leo ni huko Naples, Italy wakati Napoli ikirudiana na Mabingwa Watetezi ,Real Madrid huku wakihitaji ushindi wa bao 2-0 kwa kuwa mchezo wa awali walichapwa 3-1 huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid, Spain kwenye Mechi ya Kwanza.

Napoli pia wanaweza kufuzu ikiwa watashinda kwa idadi nyingine ya Mabao ilimradi tofauti ya Magoli iwe 2-0.

Kesho ,Jumatano Machi 8 zipo Mechi nyingine 2 ; Barcelona na Paris Saint Germain,huku PSG wakiwa mbele 4-0 na mechi ya pili ni kati ya Borussia Dortmund na Benfica huku Benfica wakiongoza 1-0.

Mechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zitakamilika Wiki ijayo, Machi 14 na 15, kwa Mechi nyingine 4 ili kutoa Washindi watakaocheza Robo Fainali.