Rostov kuwakabili Manchester United - Europa Ligi

Haki miliki ya picha Google
Image caption Wachezaji wa Fc Rostov

Michuano ya Uefa Europa Ligi inatarajia kuendelea tena Alhamisi kwa michezo mbalimbali,Apoel Nicosia watakuwa nyumbani dhidi ya Anderlecht , FC Rostov watawakaribisha Manchester United , FC Copenhagen watacheza dhidi ya Ajax , Celta Vigo itamenyana na FC Krasnodar , Schalke itachuana na Borussia Monchengladbach , Lyon wtawaalika Roma , Olympiakos itacheza dhidi ya Besiktas , na KAA Gent ya ubelgiji watakuwa nyumbani wakiwakaribisha majirani zao KRC Genk