Man City kusajili chipukizi- Msimu wa kiangazi

Haki miliki ya picha Google
Image caption Wachezaji wa Manchester City

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amesema klabu inajipanga kufanya usajili msimu wa kiangazi na wanakusudia kusajili wachezaji chipukizi wenye vipaji.

City wako kwenye hatua za katikati katika mipango yao ya kusuka kikosi chao kufuatia kuwasajili John Stones, Claudio Bravo, Leroy Sane, Ilkay Gundogan, Nolito na Gabriel Jesus kiangazi mwaka jana.

Akizungumza na wanahabari kuhusiana na suala hilo, Guardiola amesema klabu inasajili kwa ajili ya mipango ya muda mrefu ndio maana wamekuwa na wachezaji kama Raheem Sterling, Jesus na Sane.

Guardiola amesema wanaweza kuongeza mchezaji mmoja au wawili wenye umri mkubwa kwsababu ya uzoefu pindi dirisha la usajili likapofunguliwa Juni.