Pigano la Pacquiao na Amir Khan lafutiliwa mbali

Manny Pacqiuiao na Amir Khan Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Manny Pacqiuiao na Amir Khan

Bondia wa Uingereza Amir Khan hatopigana na bingwa wa uzani wa Welterweight Manny Pacquiao mwezi ujao kulingana na promota Bob Arum

Mabondia hao wawili walikuwa wametangaza pigano hilo kufanyika mnamo mwezi Aprili 28 katika mtandao wa Twitter mwisho wa mwezi Februari huku UAE ikitajwa kuwa eneo la pigano hilo.

Lakini Arum ameambia ESPN: Pigano hilo limefutiliwa mbali.

''Ninazungumzia kuhusu pendekezo jingine lakini sio Khan.Khan hatakuwa mpinzani wa Manny''.

Pigano hilo la mwezi Aprili lilipangwa baada ya mashabiki wa Paqcuiao katika mtandao wa Twitter kumpigia kura Khan kuwa mpinzani ambaye wangependelea bondia huyo mwenye umri wa miaka 38 kupigana naye.

Khan mwenye umri wa miaka 30 aliyeshinda medali ya fedha katika uzani wa Lightweight katika michezo ya Olimpiki ya 2004, alimshinda Kell Brook, raia wa Australia Jeff Horn na Mmarekani Terence Crawford kwa asilimia 48 ya kura hizo zilizofanywa na Pacquiao.