Everton kuivaa West Bromwich -Epl

Haki miliki ya picha Google
Image caption Wachezaji wa Everton

Ligi kuu ya soka la England inatarajiwa kuendelea tena kesho jumamosi kwa michezo mitatu,Bournemouth watakuwa wenyeji wa West Ham United, Everton watakuwa nyumbani dhidi ya West Bromwich Albion, na Hully city watawakaribisha Swansea city.

Idhaa ya kiswahili ya BBC Itakutangazia mchezo kati ya Everton na West Bromwich Albion.

Na Jumapili ligi hiyo itaendelea tena kwa mchezo mmoja ambapo Liverpool watakuwa nyumbani Anfield wakiikaribisha Burnley ambapo pia Idhaa ya Kiswahili ya BBC Itakutangazia mchezo huo.