Je uhusiano wa soka kwa Wenger uliodumu kwa miaka mingi unafikia kikomo?

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa Arsenal Arsene Wenger

Arsene Wenger, amehudumu kama meneja wa klabu ya Arsenal kwa miaka 21 lakini wiki hii imeweka hatma yake ya miaka ijayo katika wasiwasi kuliko wakati mwengine ule wowote katika uongozi wake.

Kubanduliwa kwa mara ya saba katika hatua ya kumi na sita bora katika ligi ya kombe la vilabu bingwa Ulaya ulikuwa uchungu wa kutosha , bila kuongeza pigo la magoli 10-2 kutoka kwa Bayern Munich.

Malalamiko dhidi ya Wenger yamekuwa yakisikika chini kwa chini kwa miaka mingi lakini sasa malalamiko hayo yameongezeka .

Kwa mwaka huu wote , mkataba mpya bado uko mezani , huku meneja huyo mwenye umri wa miaka 67 akisema maoni ya mashabiki yatachochea uamuzi wake iwapo atasalia kama meneja.

Wenger kila mara hukoselewa na vyombo vya habari, na mashabiki wengi wamezoea kupata habari na mabadiliko na sio uthabiti wake

Alisema maneno sawa na hayo yeye mwenyewe .

Liverpool hawajawahi shinda ligi ya Uingereza na Manchester United wamechukua muda tangu kushgiriki katika ligi ya Vilabu bingwa Ulaya lakini wawili hao wamekuwa na zaidi ya mameneja mmoja ndiposa hawakosolewi mara nyingi.