FA yamuongeza adhabu Mings

Zlatan Ibrahimovic Haki miliki ya picha Reuters

Difenda wa Bournemouth,Tyrone Mings ''amekasirishwa sana'' na marufuku aliyopewa ya michezo mitano kwa madai ya kumgonga kichwa Zlatan Ibrahimovic.

Kundi la wanachama wa (FA) ,limeamua kwamba Mings alimuangukia kichwani mwa mshambuliaji wa Manchester United siku ya Jumamosi walipotoka sare ya 1-1.

''Tabia kama hizo si katika mchezo wangu , haijawahi kufikiria kitu kama hicho akili mwangu ,'' Mings amesema

Ibrahimovic pia alimpiga kisukusuku Mings na akakubali marufuku ya michezo mitatu.

Kumpiga mtu kisukusuku makusudi na kumkanyanga mtu yote ni makosa yanayostahili kadi nyekundu , inayoambatana na marufuku ya michezo mitatu , lakini FA ilimuongezea adhabu katika kesi ya Mings.

FA - kuwaadhibu Ibrahimovic , Mings

Ibrahimovic apigwa marufuku mechi tatu

Bournemouth imeutaja uamuzi huo 'usiowakawaida'

Kwa watu kudhani naweza kumkanyanga mchezaji wenzangu kichwani inaudhi,Mings aliandika katika mtandao wake wa Twitter.

Nimekasirishwa na uamuzi wa FA kunipiga marufuku kwa kugongana kwa bahati mbaya.

''Mguu wangu haukubadilika na hakuna wakati nilisongeza mguu wangu kwa kichwa chake. Lengo langu ilikuwa nikurudi tena mchezoni na kukinga mpira.'' Mings

Mings atakosa michezo mitano ijayo , upande wa Eddie Howe haujapata ushindi wowote kutoka kwa michezo minane iliyoita .