FA yamuongezea adhabu Mings

Tyrone Mings na Ibrahimovic Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Tyrone Mings na Ibrahimovic

Difenda wa Bournemouth,Tyrone Mings ''amekasirishwa sana'' na marufuku aliyopewa ya michezo mitano kwa madai ya kumgonga kichwa Zlatan Ibrahimovic.

Kundi la chama cha soka England (FA) ,limeamua kwamba Mings alimuangukia kichwani mwa mshambuliaji wa Manchester United siku ya Jumamosi walipotoka sare ya 1-1.

''Tabia kama hizo si katika mchezo wangu , haijawahi kufikiria kitu kama hicho akili mwangu ,'' Mings amesema

Ibrahimovic pia alimpiga kisukusuku Mings na akakubali marufuku ya mechi mitatu.

Bournemouth imeutaja uamuzi huo kuwa usiowakawaida

''Kwa watu kudhani naweza kumkanyanga mchezaji mwenzangu kichwani inaudhi,'' Mings aliandika katika mtandao wake wa Twitter.

Nimekasirishwa na uamuzi wa FA kunipiga marufuku kwa kugongana kwa bahati mbaya.

Mguu wangu haukubadilika na hakuna wakati nilisongeza mguu wangu kwa kichwa chake. Lengo langu ilikuwa nikurudi tena mchezoni na kukinga mpira.

Mings atakosa mechi mitano ijayo , upande wa Eddie Howe haujapata ushindi wowote katika michezo minane iliyopita.