Manchester United kumkosa Rooney dhidi ya Chelsea

Manchester United hawatakuwa na mshambuliaji namba moja dhidi ya Chelsea
Image caption Manchester United hawatakuwa na mshambuliaji namba moja dhidi ya Chelsea

Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney ameondolewa katika kikosi kitakachomenyana na Chelsea katika hatua ya robo fainali kombe la FA itakayopigwa leo hii.

Rooney aligongana na mlinzi Phil Jones wakati wa mazoezi na kupata majeraha katika mguu wake, huku Zlatan Ibrahimovic akianza kutumikia adhabu yake ya kukosa michezo mitatu baada ya kumpiga kiwiko mlinzi wa Bournemouth Tyrone Mings.

Washambuliaji Anthony Martial na Marcus Rashford nao pia watakosa mchezo huo kwa kuwa ni wagonjwa.

Image caption Zlatan Ibrahimovic (kulia) nae pia atakosa mchezo huo

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anasema wachezaji wa kikosi chake wote ni wazima.

Manchester united hawatakuwa na mshambuliaji wa kikosi cha kwanza leo.