Nusu fainali Kombe la FA: Chelsea v Tottenham, Arsenal v Man City

Manchester City v Spurs 1981 FA Cup final replay Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Droo inatoa uwezekano wa marudio ya fainali ya 1981 kati ya Manchester City na Spurs, ambayo Spurs walishinda mechi ya marudiano

Mahasimu wa jiji la London Chelsea na Tottenham wamepangwa kukutana katika nusufainali Kombe la FA nchini Uingereza, Arsenal nao wakapangwa kukutana na Manchester City.

Arsenal watakuwa wanacheza nusu fainali Kombe la FA kwa mara ya 29

Nusu fainali zote mbili zitachezewa Wembley wikendi ya 22 na 23.

Chelsea walifuzu kwa kuwafunga Manchester United 1-0 Jumatatu.

Spurs walifika nusu fainali kwa kulaza Millwall 6-0 Jumapili.

Arsenal, ambao walishinda kombe hilo 2014 na 2015 waliwalemea Lincoln City 5-0 Jumamosi.

Manchester City ambao wanacheza nusu fainali kwa mara ya kwanza katika misimu minne, walifuzu kwa kulaza Middlesbrough 2-0 ugenini.

Droo ya nusu fainali:

Chelsea v Tottenham Hotspur

Arsenal v Manchester City

Matokeo ya mechi kati ya klabu zilizo nusu fainali zilipokutana
Chelsea v Tottenham
1 Machi, 2015: Chelsea 2-0 Tottenham Kombe la Ligi
29 Nov, 2015: Tottenham 0-0 Chelsea Ligi ya Premia
2 Mei, 2016: Chelsea 2-2 Tottenham Ligi ya Premia
26 Nov, 2016: Chelsea 2-1 Tottenham Ligi ya Premia
4 Jan, 2017: Tottenham 2-0 Chelsea Ligi ya Premia
Arsenal v Manchester City
13 Sep, 2014 Arsenal 2-2 Manchester City Ligi ya Premia
18 Jan, 2015: Manchester City 0-2 Arsenal Ligi ya Premia
21 Des, 2015: Arsenal 2-1 Manchester City Ligi ya Premia
8 Mei, 2016: Manchester City 2-2 Arsenal Ligi ya Premia
18 Des, 2016: Manchester City 2-1 Arsenal Ligi ya Premia

Mada zinazohusiana