Mpiganaji wa kickboxing afariki baada ya pigano

Scott Marsden mchezaji wa KickBoxing aliyefariki Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Scott Marsden mchezaji wa KickBoxing aliyefariki

Kijana mmoja wa miaka 14 anayepigana mchezo wa Kickboxing amefariki baada ya kuzirai wakati wa pigano la kuwania taji la kitaifa.

Scott Marsden alipelekwa hospitalini baada ya kuhitaji matibabu ya dharura wakati wa pigano hilo lililofanyika mjini Leeds siku ya Jumamosi, Lakini akafariki baadaye.

Scott alikuwa mwanachama wa muungano wa Marsden All Styles Kickboxing mjini Sheffiled.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Scott Marsden

Rais wa muungano wa shirikisho la mchezo wa Kickboxing duniani nchini Uingereza WKA Jon Green anasema kuwa Scott alikuwa mpiganaji anayeheshimiwa sana na mchezaji maarufu.

Maafisa wa Polisi wa West Yorkshir alisema kuwa maafisa walikuwa wanachunguza kilichotokea lakini kifo chake kilikuwa kikichukuliwa kisicho na shuku.

Mada zinazohusiana