Leicester yatinga robo fainali UEFA

Leicester City wameifunga Sevilla magoli 2-0 na kuingia robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya, kwa jumla ya magoli 3-2 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa King Power.

Haki miliki ya picha TIM KEETON
Image caption Marc Albrighton akisherekea baada ya kufunga bao la pili

Nahodha wa Leicester Wes Morgan alipachika bao la kwanza katika dakika ya 27, na kufanya matokeo kuwa ya sare ya 2-2 dhidi ya Sevilla ambao walionekana kutocheza kwa kuelewana.

Marc Albrighton alifunga goli muhimu la pili mapema katika kipindi cha pili, kabla ya kiungo Samir Nasri kuoneshwa kadi ya pili ya manjano na kutolewa nje.

Haki miliki ya picha Laurence Griffiths
Image caption Samir Nasri alitolewa baada ya kuzozana na Jamie Vardy

Licha ya kucheza pungufu, Sevilla walipoteza nafasi ya kuupeleka mchezo katika muda wa ziada baada ya Kasper Schmeichel kuokoa mkwaju wa penati uliopigwa na Steven Nzonzi.

Juventus yasonga

Katika mchezo mwingine, Juventus walisonga mbele kwenda robo fainali kwa kuilaza Porto bao 1-0.

Paulo Dyabala alifunga bao hilo pekee kwa mkwaju wa penati kufuatia Pereira kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Pereira alitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Droo ya robo fainali itafanyika siku ya Ijumaa Machi 17.