Manchester United yashtakiwa na FA

Wachezaji wa Manchester United wakimzunguka refa Oliver baada ya kumuonyesha kadi nyekundu Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Wachezaji wa Manchester United wakimzunguka refa Oliver baada ya kumuonyesha kadi nyekundu

Klabu ya Manchester United imeshtakiwa na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake wakati wa mechi ya robo fainali ya kombe la FA siku ya Jumamosi dhidi ya Chelsea.

Refa Michael Oliver alizungukwa na wachezaji wa United baada ya kumpa kadi nyekundu Ander Herrera dakika 10 kabla ya muda wa mapumziko.

United ilipoteza mechi hiyo kwa 1-0.

Taarifa ya FA ilisema kuwa United ina hadi saa kumi na mbili jioni saa za Uingereza kujibu.

Kiungo wa kati wa Uhispania Herrera alitolewa nje baada ya kumchezea visivyo kwa mara ya pili mshambuliaji Eden Hazard.

Hakuna hatua zaidi itakayochukuliwa dhidi ya Marcos Rojo a kisa alichofanya katika dakika za mwisho za mechi.

Rojo alionekana akimkanyaga Hazard.