UEFA: Samir Nasri amlaumu Jamie Vardy kwa kadi nyekundu

Samir Nasri na Jamie Vardy Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Samir Nasri na Jamie Vardy wakikaripiana wakati wa mechi

Kiungo wa kati wa Sevilla Samir Nasri amemtuhumu Jamie Vardy kwa kutumia hila kutokana na kadi nyekundu aliyopatiwa siku ya Jumanne katika mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Nasri, 29, alitolewa nje ya uwanja baada ya kupewa kadi ya pili ya manjano .

Leicester walifanikiwa kufuzu kwa robo fainali kwa ushindi wa magoli 3-2.

Nasri na Vardy waligongana vichwa katika kipindi cha pili cha mchezo.

Nasri ambaye ametoka Manchester City kwa mkopo anaamini hatua ya Vardy kujionesha kana kwamba alikuwa ameumizwa ilimfanya mwamuzi Daniele Orsato kuchukua hatua hiyo.

''Kwangu mimi ni muongo, kwa sababu angekuwa mchezaji wa kutoka nchi za nje, nyinyi wanahabari wa Uingereza mngekuwa mkisema ni muongo,'' Nasri alisema.

"Walikuwa wanashinda kwa magoli 2-0 , cheza mchezo kama mwanamume. Hamko bora kutushinda sisi lakini mnashinda 2-0 na mtafuzu, chezeni mchezo."

Lakini mshambuliaji huyo raia wa Uingereza, Vardy alipinga madai ya Nasri na kusema "mimi si muongo na wala sitakuwa muongo. Hayo ndiyo ninayoweza kusema kuhusiana na suala hili.''

Msemaji wa Leicester aliongeza: Klabu hiyo ilipinga madai yote wanayohusiana na uadilifu wa mchezaji Jamie ama mchezaji yoyote yule wa klabu hiyo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Samir Nasri akikataa kuondoka uwanjani baada ya kupokea kadi ya manjano ya pili.

Sevilla walikuwa wamepokea kichapo cha magoli 2-0, magoli yakitoka kwa Wes Morgan na Marc Albrighton.

Na walilazimishwa kucheza dakika 20 za mwisho na wachezaji 10 wakiendelea kutafuta bao muhimu la kuwawezesha kufuzu.

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ufaransa Nasri alisindikizwa nje ya uwanja na wachezaji wenza, na walichukua zaidi ya dakika tatu za mchezo.

"Kwa mchezaji wa kimataifa hastahili kufanya hivyo, angalia picha hiyo. Kweli alivyofanya hivyo, lakini alifanya kwa ustadi," alisema

''Nilidhani wachezaji wa Uingereza walikuwa na ukakamavu zaidi. Alikuja mbele ya uso wangu.

Ilikuwa ikabu na akanisukuma, na nikamwuliza anafanya nini? Hapo ndipo alikuja mbele ya uso wangu . Hivyo ndivyo ilivyokuwa.

Nikisema ukweli sidhani hivyo ndivyo mtakavyoandika. Ningependa kuzungumza naye, kuna kamera nyingi na usalama umeimarishwa na ni wajibu wangu kufikiria mwaka ujao na si kufikiria kuhusu marufuku."