Guardiola: Nilishindwa kuwashawishi wachezaji wangu kushambulia

Pep Guardiola asema alishindwa kuwashawishi wachezaji wake kushambulia
Image caption Pep Guardiola asema alishindwa kuwashawishi wachezaji wake kushambulia

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa kushindwa kwake kuwashawishi wachezaji wa Manchester City kufanya mashambulio dhidi ya Monaco ndio chanzo cha wao kutolewa katika kombe la vilabu bingwa.

Wakiwa na uongozi wa 5-3 baada ya awamu ya kwanza ya mechi ya muondoano wa timu 16, City ilichezesha wachezaji kumi na moja kwa lengo la kushambulia katika awamu ya pili siku ya Jumatano lakini wakapoteza 3-1 na hivyobasi kutolewa na bao la ugenini.

''Nilijaribu kuwashawishi wachezaji wangu katika mikutano yote kwamba tunafaa kushambulia ili kupata bao'',alisema Guardiola.

''Makosa yangu ni kushindwa kuwashawishi kufanya hivyo''.

Raia huyo wa Uhispania aliongeza:Nilifanya hivyo katika kipindi cha pili lakini ikawa tumechelewa.

''Wakufunzi wote hufanya makosa lakini sidhani kwamba ni mbinu tuliotumia''.