Slaven Bilic: Ulikuwa uamuzi "mbaya" kumfuta Ranieri

Claudio Ranieri Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Leicester ilimfuta Claudio Ranieri (kushoto) mwezi Februari

Meneja wa West Ham, Slaven Bilic, amesema ulikuwa uamuzi ''mbaya''kwa klabu ya Leicester City kumpiga kalamu Claudio Ranieri lakini umethibitishwa na matokeo yao.

Mabigwa hao watetezi wa klabu bigwa ulaya , hawajapoteza mechi yoyote tangu Ranieri, 65, alipopigwa kalamu mwezi Februari.

Pia waliweza kufika robo fainali ya ligi ya Champions baada ya kupata ushindi dhidi ya Sevilla.

''Hakuna mtu anayeweza kusema ulikuwa uamuzi mbaya, matokea matatu ya hivi majuzi yamekuwa yakupendeza,''Bilic alisema.

''Lakini kwangu mimi bado ulikuwa uamuzi mbaya , Claudio aliwaheshimu.

Ranieri aliwaongoza Leicester, kwa ushindi uliowashangaza wengi kwa kulinyakua taji ya Premia mwaka 2016, lakini The Foxes walikuwa alama moja juu ya hatua ya muondoano na walikuwa wamepoteza michezo mitano ya ligi kabla ya kufutwa kwake.

Leicester ilikuwa haijafunga goli lolote mwaka 2017, na wamefunga magoli saba katika mechi tatu walizoshiriki chini ya uongozi wa Craig Shakespeare ambaye anaiongoza timu hiyo hadi mwisho wa msimu huu.

''Nilisema baada ya kumbadilisha meneja , kile nilichofikiria na bado sijalielewa swala hilo," Bilic amesema.''

''Lakini ukizungumzia matokeo na jitihada zao , walipata walichotaka.''

West Ham wako katika nafasi ya 11 katika ligi ya klabu bingwa, watakutana na the Foxes siku ya Jumamosi uwanjani Stadium.