Arsenal yatwangwa na West Brom Albion

Arsenal ilishindwa kwa mabao 3-1
Image caption Arsenal ilishindwa kwa mabao 3-1

Arsenal ilipata pigo la nne katika mechi tano za ligi baada ya mabao mawili ya Craig Dawson kuisaidia West Bromwhich Albion kuilaza timu hiyo ya Arsene Wenger kwa mabao 3-1.

Dawson alitumia fursa ya makosa yaliofanywa na walinda lango la Arsenal kufunga mabao yake yote mawili kwa kichwa kupitia kona zilizopigwa na hivyobasi kuathiri uwezo wa Arsenal wa kumaliza katika timu nne bora.

Awali Arsenal ilikuwa imejikakamua baada ya kuwa bao moja chini ,na kusawazisha kupitia Alexi Sanchez likiwa bao la 18 la mchezaji huyo wa Chile msimu huu.

Hatahivyo walisalia nyuma kwa mara ya pili dakika kumi za kipindi cha pili baada ya mchezaji wa ziada Hal Robson Kanu kufunga bao, dakika mbili tu baada ya kuingia.

Arsenal ambayo ilimpoteza kipa Petr Cech kupitia jeraha walikabiliwa na kutawaliwa na kushindwa kupata bao la pili.

Na mwisho wamechi hiyo mashabiki wa timu ya Arsenal waliendelea jitihada za za kumtaka kocha wa klabu hiyo kufutwa kazi kwa matokeo mabaya.

Walibeba mabongo yaliomtaka kocha huyo kuondoka