Mchezaji ajikanganya kwa kumshukuru mkewe pamoja na ''girlfriend''

Mohammed Anas mchezaji wa Ghana aliyejikanganya na kupata umaarufu mkubwa
Image caption Mohammed Anas mchezaji wa Ghana aliyejikanganya na kupata umaarufu mkubwa

Mchezaji mmoja wa soka ambaye katika mahojiano yake baada ya mechi alimshukuru mkewe pamoja na rafikiye wa kike {Girlfriend} wa kando amekana kutokuwa mwaminifu katika ndoa yake.

Mohammed Anas kutoka Ghana wa klabu ya soka ya Free State Stars aliambia BBC alikuwa akizungumzia kuhusu mwanawe wa kike.

''Familia yangu inajua kwamba ninamuita mwanangu wa kike 'Girlfriend'.

Anas anasema kuwa hajali kuhusu hisia za mkewe baada ya mahojiano hayo .

Anasema ameshangazwa na idadi ya watu waliotazama kanda hiyo.

''Mimi ni maarufu sasa, watu duniani kote wananijua''.

Aliongezea: Nimekuwa na mke wangu ambaye ni raia wa Afrika Kusini kwa miaka .

''Ninampenda sana. Amenipatia watoto wawili warembo sana .Yuko salama. Anajua nilivyo na kwa hivyo sina wasiwasi'', alisema.

Anas alikanganyika baada ya kuhojiwa kuhusu mchezo wake mzuri uliomfanya kupewa taji la mchezaj bora wa mechi ambapo timu yake ilitoka sare ya 2-2 na klabu ya Ajax kutoka Cape Town.

Katika mahojaino hayo,mchezaji huyo alisema: Asante sana kwa kunipatia hili.na nawashukuru mashabiki wangu mke wangu na rafiki yangu wa kike{Girlfriend} ....''Alijisahihisha kwa kwa kusema: Ninamaanisha mke wangu pole kwa kusema hivyo pole mke wangu''.

Kanda hiyo ya video imesambazwa mara 25,000 katika mtandao wa You Tube pamoja na mitandao mengine ya kijamii.