Dawa za kupunguza maumivu ni hatari kwa maisha ya wanasoka

Dawa ya kupunguza maumivu Haki miliki ya picha SPL
Image caption Dawa ya kupunguza maumivu Ibuprofen

Kundi la wataalam la wachezaji wa soka, 'hutumia vibaya' dawa zilizoruhusiwa za kupunguza maumivu na 'zinauwezo' wa kusababisha madhara maishani , amesema afisa mkuu wa afya wa zamani wa Fifa.

Karibu nusu ya wachezaji waliokuwa wakishiriki michuano ya kombe la taifa kwa miaka mitatu iliyopita wamekuwa wakitumia dawa hizo mara kwa mara kama vile Ibruprofen , amedai Jiri Dvorak

Amesema bado ni mfumo unaoongezeka miongoni mwa wachezaji ikiwemo vijana.

''Limekuwa swala la kitamaduni katika mchezo," amesema Profesa Dvorak.

''Ni kosa kabisa , aliongeza, Czesh, aliyeianga Fifa mwezi Novemba baada ya kuhudumu kwa miaka 22.

''Kwangu mimi ni wazi kwamba watu wanatumia dawa hizo vibaya , ndio maana kulitumika neno la onya.''

Hata hivyo, muungano wa wachezaji wa soka wa kulipwa , muungano wa wachezaji wa England wamesema matumizi mabaya ya dawa hizo za kupunguza makali , si jambo kubwa miongoni mwa wachezaji wake.

Image caption Mchambuzi wa BBC na beki wa zamani wa Kimataifa wa England Danny Mills

Mchambuzi wa BBC na beki wa zamani wa Kimataifa wa England Danny Mills amesema dawa hizo za kupunguza maumivu kwenye soka zimetumika kwa wingi ''na bado zitakuwepo''

Nimekuwa katika vyumba vingi vya wachezaji vya kubadilishia nguo , ambapo nimewaona wachezaji wengine walikilazimishwa kutumia dawa hizo wanapokuwa uwanjani, amesema.

Aliongeza wachezaji wa viwango vya juu katika mchezo hawakuchukulii dawa hizo kama tatizo kwa sababu zilikuwa zimeidhinishwa na zilikuwa zikidhibitiwa na wataalam wa afya lakini alihisi wachezaji wengine katika hadhi ya chini katika ligi wanauwezo wa kutaabika iwapo usalama hautazingatiwa.

Profesa Dvorak alizungumza na BBC katika Makala ya wiki ya State of Sport , ambayo siku ya Alhamisi itaangazia usawa wa maslahi ya wanariadha dhidi ya tamaduni za ushindi wa aina yoyote kwenye michezo.

Kamati ya serikali ya ukaguzi itaangazia usalama na maslahi ya wanamichezo wa Uingereza , ikiongozwa na bingwa wa mara 11 wa michezo ya Paralympic ,Baroness Grey-Thompson inayotarajiwa kuchapishwa kwa haraka.

Profesa Dvorak alikusanya data kuhusiana na viwango vya dawa vinavyotumiwa na wachezaji katika kila michuano ya Fifa kati ya mwaka 1998 na 2014 na kubaini asilimia 50 hutumia dawa hizo 'kila siku' za kupunguza maumivu zinazopatikana kwenye maduka ya dawa.

Amesema klabu nyengine huangazia ushindi kuliko maslahi ya wachezaji wake , na kuwasababishia wachezaji wake kupata 'msukumu' wakutumia dawa hizo kujiepusha na majeraha madogo ili kucheza michuano muhimu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Profesa Dvorak

Profesa Dvorak hapo awali alielezea wasiwasi wake alipoajiriwa na Fifa lakini anadai kwamba bodi ya kimataifa bado haijaangazia swala hilo sawasawa.

Fifa imesema misimamo yake kuhusiana na swala hilo bado halijabadilika tangu Dvorak alipotoa tahadhari mara ya kwanza kuhusiana na madhara ya kudumu kuhusiana na matumizi ya dawa hizo kwa wachezaji mwaka 2012.

Matumizi mabaya ya dawa zilizohalalishwa zinauwezo wa kuwasababisha wachezaji kupata shida za kuhatarisha maisha ,amedai Profesa Drovak.

''Tunastahili kutoa taarifa kali kwa wachezaji :Waamke na wawe waangalifu , alisema. Hazina hatari yoyote na ndio maana mnafikiria mnauwezo wa kuzila kama biskuti .zinamadhara yake.''