Lewis Hamilton amshinda Vettel Australia Grand Prix

Mashindano ya magari ya langalanga ya Australia Grand Prix Haki miliki ya picha AP
Image caption Mashindano ya magari ya langalanga ya Australia Grand Prix

Lewis Hamilton alishinda taji lililokuwa na ushindani mkali kati ya Mercedes na Ferrari katika mashindano ya magari ya langalanga ya Australia Grand Prix.

Muingereza Hamilton alishinda taji hilo kwa sekunde 0.268 huku Dereva wa Ferrari Sebastian Vettel akijiunga naye.

Mjerumani huyo alimshinda mshindabi mwenza wa Hamilton Valteri Bottas kwa sekunde 0.025 huku msimu mpya wa magari yenye kasi ya juu ukianza vizuri.

Kimi Raikkonen wa Ferrari alichukua nafasi ya nne mbele ya dereva wa gari la Red Bull Max Verstappen.