Kocha wa zamani wa Ghana aondoka hotelini baada ya wiki 7

Kocha wa zamani wa Ghana aondoka hotelini baada ya wiki 7
Image caption Kocha wa zamani wa Ghana aondoka hotelini baada ya wiki 7

Aliyekuwa kocha wa kiikosi cha Ghana Gerard Nus, ameondoka hotelini baada ya wiki saba kufuatia shirikisho la kandanda nchini humo kumlipa marupurupu yake.

Amekuwa akikataa kuondoka kwenye hoteli hiyo iliyo mjini Accra, tangu yamalizike mashindano ya kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika mapema mwezi Februari.

Shirikisho la kandanda nchini Ghana (GFA) linasema lilifanikiwa kupata pesa na kumlipa marupurupu yake yote siku ya Jumamosi.

Raia huyo wa Uhispania kisha ameondoka Ghana leo na kurudi kwa Uhispania.

"Nawashukuru watu wote nchini Ghana. Kumbukumbu nzuri kutoka kwa taifa hili tukufu linaloipenda kandanda.

Kulingana na taarifa ya GFA, kulikuwa na mvutano kuhusu ni nani angelipia gharama ya hoteli ambapo Nus alikuwa akiishi.