Uwanja wa ndege waitwa jina la Ronaldo Ureno

Muonekano wa uwanja wa Madeira kwa sasa
Image caption Muonekano wa uwanja wa Madeira kwa sasa

Licha ya kupoteza 2-1 dhidi ya Sweden Ronaldo ataondoka kwa ufahari nchini mwake baada ya uwanja wa ndege wa Madeira sehemu aliyozaliwa kubadiliwha njina na kuwa uwanja wa ndege wa Cristiano Ronaldo

Ureno walianza kupata goli baada ya mlinzi wa Sweden Andreas Granqvist kujifunga mwenyewe dakika ya 71.

Viktor Claesson akaiandikia Sweden goli la kwanza kabla ya Cavaco Cancelo kujifunga muda wa majeruhi.

Ronaldo anatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuitwa jina hilo siku ya Jumatano.

Image caption Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji wenye historia ya kuvutia zaidi Ureno

Mchezaji huyo mwenye miaka 32 aliyeingoza timu yake ya taifa kutwaa kombe la mataifa ya Ulaya 2016, amezaliwa katika mji wa Madeira katika kitongoji cha Funchal, kabla ya kujiunga na timu ya Lisbon na baadaye Manchester United.

Baadhi ya wanasiasa wamepinga uamuzi wa kubadili jina la uwanja wa ndege wa Maderia kuitwa Cristiano Ronaldo Airport.