Sanamu ya kushangaza ya Cristiano Ronaldo yazinduliwa Ureno

Ronaldo Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ronaldo akipigwa picha na sanamu hiyo Jumatano

Mashabiki wengi wa mchezo wa kandanda dniani wameshangazwa na sanamu ya mchezaji nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ambayo ilizinduliwa katika kisiwa cha Madeira nchini Ureno.

Sanamu hiyo ilizinduliwa wakati wa sherehe ya kuupa jina uwanja wa Madeira ambao sasa umekuwa Uwanja wa Cristiano Ronaldo.

Wengi katika mitandao ya kijamii wanasema sanamu hiyo inafanana sana na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland Niall Quinn badala Ronaldo.

Waziri mkuu wa Ureno alihudhuria sherehe hiyo ya kuupa jina uwanja huo wa Madeira na ndiye aliyezindua sanamu hiyo.

Image caption Baadhi wanasema sanamu hiyo inafanana zaidi na Niall Quinn
Haki miliki ya picha @mrdanwalker

Rais wa Ureno Rebelo de Sousa alisema Ronaldo "amekuwa akitangaza Madeira na Ureno maeneo ya mbali zaidi duniani kuliko mtu mwingine yeyote."

Ronaldo, 32, huchukuliwa kama shujaa Madeira, ambapo anatazamwa kama mfano mwema kwa mtu aliyeanzia maisha katika ufukara hadi akawa tajiri.

Tayari ana makumbusho yaliyopewa jina lake katika mji wake wa kuzaliwa wa Funchal.

Mchezaji huyo baadaye aliandika kwenye Twitter: "Nina furaha isiyo na kifani na ni heshima kubwa jina langu kuwa kwenye uwanja wa Madeira!"

Ronaldo si mchezaji wa kwanza kuwa na uwanja ambao umepewa jina lake.

Uwanaj wa ndege wa Belfast ulipewa jina la mchezaji wa zamani wa Manchester United George Best mwaka 2006, mwaka mmoja baada yake kufariki dunia.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Sanamu ya Cristiano Ronaldo ilizinduliwa katika uwanja wa ndege wa Madeira
Haki miliki ya picha AP

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii