Diego Maradona ashtaki kampuni kuhusu mchezo

The striking likeness Haki miliki ya picha PES 2017

Diego Maradona amesema kwamba atashtaki kampuni ya Konami inayomiliki mchezo wa video kwenye kompyuta wa Pro Evolution Soccer.

Mchezaji huyo kutoka Argentina amekasirishwa na hatua ya walioutunga mchezo huo kutumia sura inayofanana na yake kwenye mmoja wa wahusika kwenye mchezo huo bila idhini.

Kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema wakili wake "atachukua hatua zifaazo za kisheria" dhidi ya kampuni hiyo ya Japan.

Nyota huyo aliyewahi kuchezea Barcelona na Napoli kama kiungo wa kati ameongeza kwamba anatumai huo si mpango mwingine wa kuwapora watu pesa mtandaoni.

Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Ujumbe wa Maradona kwenye Facebook

Unapokuwa unacheza mchezo huo katika kitengo cha myClub Maradona anatokea miongoni mwa wachezaji bingwa wastaafu.

Wengine ni pamoja na Henrik Larsson, Thierry Henry na Gary Lineker.

Maradona ana alama 98, ya juu zaidi. Ronaldo ana 93 na Ronaldinho alama 91.

Haki miliki ya picha PES 2017

Pro Evo ni moja ya michezo maarufu sana iliyoundwa na Konami na mchezo huo umekuwa ukiuzwa tangu 2003.

Ni muundo mpya wa mchezo wa awali wa International Superstar Soccer ambao ulianza 1995.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii