Mourinho: Manchester United watawakosa Chris Smalling na Phil Jones muda mrefu

Phil Jones na Chris Smalling Haki miliki ya picha Empics
Image caption Phil Jones (pili kushoto) anaonekana kuumia baada ya kukabiliwa na Chris Smalling (kati) wakati wa mazoezi

Mabeki wa Manchester United Chris Smalling na Phil Jones walipata majeraha ya kuwaweka nje kwa muda mrefu walipokuwa wanachezea timu ya taifa ya England, meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho amesema.

Jones, 25, aliumia kwenye kidole wakati wa mazoezi akikabana na mpinzani.

Taarifa zinasema kisa hicho kilimhusisha Smalling.

Beki mwenzake Smalling, 27, alipigwa picha akiwa amefungwa kitambaa mguuni baada ya kuumia pia wakati wa mazoezi.

'Yuda' Mourinho 'bado anaongoza Chelsea'

Nahodha wa United Wayne Rooney hata hivyo amepata nafuuu na atarejea kuwachezea dhidi ya West Brom Jumamosi baada ya kupona jeraha la goti.

Rooney, 31, alikosa mechi United za karibuni zaidi walizocheza United.

Kutokana na kuumia kwa Smalling na Jones, Mourinho amemwita beki wa miaka 19 Axel Tuanzebe kikosini kwa ajili ya mechi hiyo.

Tuanzebe amechezea United mechi moja pekee ya ushindani, mechi ambayo walilaza Wigan 4-0 katika Kombe la FA Januari.

United watakuwa pia bila mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na kiungo wa kati Ander Herrera wanaoumikia marufuku.

Pia, watamkosa Paul Pogba, anayeuguza jeraha la misuli ya paja.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii