Liverpool yaitandika Everton 3-1

Liverpool yaitandika Everton 3-1 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Liverpool yaitandika Everton 3-1

Liverpool iliongezea matumaini ya kuendelea kusalia katika kundi la timu nne bora baada ya kuwatandika Everton mabao 3-1 katika Champions League.

Sadio Mane aliwapa Liverpool bao la mapema kufuatia ushirikiano mzuri na Roberto Firmino.

Bao la pili lilifungwa na Philipe Coutinho baada ya kuwabwaga wachezaji wawili wa Everton.

Matokeo hayo yanaipa Liverpool uongozi wa pointi 7 mbele ya nambari tano Manchester United, ambao wana mechi tatu za kucheza, ikiwemo ya nyumbani dhidi ya West Brom siku ya Jumapili.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Philippe Coutinho