Arsenal yatoka sare ya 2-2 na Manchester City

Arsenal yatoka sare ya mabao 2 na Manchester City Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Arsenal yatoka sare ya mabao 2 na Manchester City

Arsenal ilijitahidi mara mbili ikasawazisha na kutoka sare ya mabao mawili na Manchester City, matokeo ambayo yanaiweka nyuma ya City kwa pointi saba.

Kiungo wa mbele Leroy Sane, aliwafungia wageni bao la kwanza dakika tano baada ya kuanza kwa mechi, lakini Theo Walcott akawaokoa Arsenal na kusawazisha bao hilo.

Hata Sergio Aguero alikifungia kikosi cha Pep Guardiola takriban dakika mbili baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.

Naye Shkodran Mustafi alitumia fursa ya kona iliyochongwa na Mesut Ozil na kusawazisha mabao 2.

Huku hatma ya meneja Arsene Wenger ikiwa haijulikani, sare hiyo inaicha Arsenal katika nafasi ya sita licha ya kubaki na mechi kadha za kucheza.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pep Guardiola na vijana wake

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii