Serengeti boys watoshana nguvu na Black Starlets

Haki miliki ya picha Google
Image caption Serengeti boys

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania Serengeti boys wakicheza katika dimba la taifa jijini Dar wameenda sare ya mabao 2-2 na timu ya vijana ya Ghana .

Katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki Ghana ama black Starlets ndio walianza kuziona nyavu za Serengeti kwa mabao ya Sulley Ibrahimu dakika ya 30 na Arko Mensah dakika ya 73.

Serengeti walisawazisha magoli hayo kupitia kwa Asad Juma kwa penalti na Muhsin Malima mabao yote yakifungwa dakika za nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida za mchezo.

Huo ulikuwa mchezo wa tatu wa majaribio katika maandalizi ya Serengeti Boys kujianda na fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, michuano itayofanyika nchini Gabon.